top of page

SAUTI YA MTOTO: KILIO KISICHOSIKIKA

Updated: May 4

Katika ulimwengu wa leo wa mbio, teknolojia, na majukumu yasiyo na mwisho, sauti ya mtoto inazidi kufifia. Sauti hiyo haisikiki kwa sababu ya kelele za simu janja, michezo ya video, au kushabikia timu fulani za mpira. Lakini iko pale — dhaifu, ikilia, ikisihi, ikilia kimyakimya ndani ya mioyo yao midogo ikisema;

Mtoto wa karne hii akiwa na huzuni ya ndani isiyoelezeka — kilio kisichosikika cha kutamani upendo na uangalizi wa mzazi.
Mtoto wa karne hii akiwa na huzuni ya ndani isiyoelezeka — kilio kisichosikika cha kutamani upendo na uangalizi wa mzazi.
"Nilinde, nitunze, nivishe, nilishe, nihurumie, nisomeshe, nipeleke shule, nielekeze, tenga muda wa kucheza, kuzungumza na kukaa nami. Natamani ningekuwa hiyo smartphone yako, au game lako, au timu yako ya mpira…”

Sauti hii ya ndani si hadithi ya mbali, bali ni ukweli wa maelfu ya watoto wa karne hii. Wanalia si kwa sauti bali kwa ishara za nje kimatendo, mihemko yao, na mara nyingine kwa ukimya wao.


Lakini je, sisi kama wazazi tunasikia?


DUNIA YA LEO: TEKNOLOJIA INAVYOPORA UHUSIANO


Kwa kila dakika tunayopoteza tukiwa tumezamia simu, tunatengeneza pengo kati yetu na watoto wetu. Mara nyingi, tunawapa watoto zawadi za kifahari au vifaa vya kielektroniki tukidhani tumefidia upendo na uangalizi tunaokosa kuwapa.Lakini wao hawahitaji iPad mpya. Hawahitaji PS5. Wanahitaji sisi.

Ujumbe wa Mtoto kwa Baba, Mama na Jamii
Ujumbe wa Mtoto kwa Baba, Mama na Jamii

Mtoto anapotamka kwa sauti au kwa muonekano:

  • "Nihurumie" – Anaomba upendo usio na masharti.

  • "Nisomeshe" – Anaomba uwekezaji wa muda, si pesa pekee.

  • "Nielekeze" – Anahitaji msaada kuelewa dunia inayomzunguka.

  • "Tenga muda wa kucheza nami" – Anapenda kuwepo kwako, na si vitu vyako.

  • "Natamani ningekuwa hiyo timu ya mpira" – Anaona mapenzi yako kwa timu kuliko kwake.

Haya si maneno matupu — ni vilio vya nafsi vinavyoomba nafasi katika maisha yetu.


MAJUTO YA BAADAYE: JE, UTASEMA "LAITI..."?


Miaka isiyozuilika itapita. Mtoto atakua, atabadilika, atajifunza kuishi bila sisi. Na sisi, tukizinduka, tutajikuta tukisema:

  • "Laiti ningesikiliza zaidi."

  • "Laiti ningekaa chini kucheza naye."

  • "Laiti ningetenga muda wa kuzungumza naye, si kuangalia simu yangu."

Kwa nini tusikie sasa kabla majuto hayajawa sehemu ya historia yetu?


Na kwa sababu hawakuonja ule UWEPO wetu kwao (emotional, physical and mental attachment), nao watakuja bize na shughuli zao, na watatupeleka sisi wazazi katika nyumba za kulea wazee ili nao wawe huru na mambo yao. Watabaki wakilipa pesa za matunzo katika nyumba hizo na kuja kutembelea mara chake.


SULUHISHO: KUISHI SASA, KUSIKILIZA SASA


Kusikia sauti ya mtoto si kazi ngumu kama tunavyofikiri:

  • Weka simu chini unapokuwa nyumbani.

  • Panga ratiba ya kucheza pamoja, hata dakika 20 kwa siku.

  • Zungumza naye kama rafiki — usisikilize kwa lengo la kujibu, sikiliza kwa kuelewa.

  • Mwambie "Nakupenda" bila kusubiri sababu.

  • Onyesha kuwa anakuhusu kwa vitendo na maneno.


Kwa kufanya hivi, tunajenga kizazi kinachohisi kuthaminiwa, kueleweka, na kupendwa — si kwa vitu, bali kwa uwepo wetu.


Je, Unataka Kujifunza Zaidi Jinsi ya Kusikia Sauti ya Mtoto Wako?


Kupitia uanachama wetu wa bure au wa kulipia kwa gharama ndogo sana, ambapo gharama ya chini ni sifuri (Tsh.0, ya ofa) na ya juu ni Tsh.10,000/-, tunakupa:

  • Mwongozo wa kina wa kujenga mawasiliano bora na mtoto wako.

  • Mafunzo ya kila wiki kwa wazazi wa karne hii.

  • Majibu ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa malezi na saikolojia ya watoto.

  • Jamii ya wazazi wenzako wanaotafuta kuwa bora kila siku.

Usikubali sauti hii itoweke — jiunge nasi leo na ujifunze kusikia na kuishi upendo wa kweli wa familia yako.

Bonyeza hapa kujiunga sasa — usikose nafasi ya kubadilisha maisha ya mtoto wako!

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page