Karibu
SOHEECO Projects
Tunaboresha Maisha ya Mtu Binafsi, Jamii, Shule/ taasisi na Familia.
Kuhusu SOHEECO Projects
Karibu SOHEECO Projects – mahali ambapo mabadiliko hukutana na mafanikio! Unadhani ni UTANI? Endelea kusoma na kutufatilia!
Dhamira yetu ni kuhamasisha, kuelimisha, na kuwawezesha watu binafsi, jamii, shule, na taasisi nyingine katika nyanja za Kijamii, Afya, na Uchumi (SOHEECO). Sisi ni chanzo kinachoaminika cha mwongozo wa vitendo na suluhisho bunifu zilizobuniwa mahsusi ili kuimarisha mahusiano, kuboresha afya, na kufanikisha mafanikio ya kiuchumi.
KIJAMII: Mahusiano, Ndoa na Familia
Tunaamini kuwa mahusiano imara ndiyo msingi wa jamii zinazostawi. Maeneo yetu ya mkazo ni:
-
Ushauri wa Ndoa na Mahusiano: Kuimarisha uaminifu na mawasiliano.
-
Mienendo ya Familia: Kutatua migogoro na kujenga mazingira ya nyumbani yenye afya.
-
Ustawi wa Hisia: Kujenga ustahimilivu kupitia changamoto za maisha.
KIAFYA: Ustawi na Lishe
Afya njema ni nguzo ya ustawi wa maisha. Tunatoa huduma na elimu kuhusu:
-
Kinga dhidi ya Magonjwa: Kupunguza hatari za kiafya kwa mikakati ya vitendo.
-
Lishe Bora: Kufuata mlo kamili na tabia endelevu za ulaji.
-
Tiba Asilia: Kuzitumia kikamilifu mbinu za kiafya za asili.
KIUCHUMI: Uhasibu, Fedha, Kilimo, Uchumi wenyewe, Manunuzi, Usimamizi, na Biashara/ Ujasiriamali
Mafanikio ya kiuchumi huanzia na mikakati sahihi na usimamizi bora. Tunashughulikia maeneo yafuatayo:
-
Uhasibu na Fedha: Uandaaji wa bajeti, uhasibu wa kila siku, na uzingatiaji wa sheria za kodi kwa watu binafsi na wafanyabiashara.
-
Kilimo: Kilimo endelevu, usimamizi wa mazao, na matumizi ya mbinu bunifu kwa wakulima.
-
Uchumi: Uelewa wa masoko, mwenendo wa kiuchumi, na athari za sera.
-
Manunuzi: Usimamizi wa rasilimali kwa ufanisi na mikakati ya mnyororo wa ugavi.
-
Usimamizi: Ujuzi wa uongozi, mikakati ya uendeshaji wa taasisi, na kufanya maamuzi yenye tija.
-
Ujasiriamali: Kuanza na kukuza biashara hata kwa rasilimali chache.
Katika SOHEECO Projects, tunachanganya utaalamu kutoka miradi yetu hii:
-
ACAMABECA ENTERPRISE (inayolenga kukuza uchumi), na
-
FUHUWI CONSULTATION CENTRE (inayojikita kwenye masuala ya kijamii na kiafya).
Pamoja, tunakuwezesha kufanikisha mabadiliko ya maana katika kila nyanja ya maisha.
Karibu tupige hatua kwa pamoja — hatua moja karibu zaidi na maelewano ya kijamii, afya bora, na uhuru wa kiuchumi.
Jiunge nasi katika kujenga maisha yenye afya, nguvu na mafanikio zaidi!
KUTANA NA TIMU YETU

Francisco J. Kagoma
Mwasisi (Founder) na Mkurugenzi (CEO) | SOHEECO PROJECTS
Ni mtaalamu wa uhasibu na usimamizi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 6 katika shule binafsi. Kupitia SOHEECO PROJECTS yaani FUHUWI CONSULTATION CENTRE na ACAMABECA ENTERPRISE, amejikita katika kutoa maarifa ya kiutawala, kifedha, kiuchumi, na maendeleo ya taasisi kwa njia ya elimu, ushauri na maandiko ya kitaalamu. Pia anatoa maarifa na ushauri kuhusu lishe bora, magonjwa yasiyombuzika, mahusiano, ndoa na familia. Pia ni Mbunifu wa Tovuti (Website Designer) ya SOHEECO Projects. Tovuti ya SOHEECO Projects ni moja ya kazi zake (https://www.soheecoprojects.com)
Ni mume wa mke mmoja (1) na watoto wawili (2).

Sylvia Temu
Mkurugenzi Msaidizi (Deputy CEO) | SOHEECO PROJECTS
Ni mzoefu mkubwa katika masuala ya ujasiriamali, ya kujitolea kwa huduma za kijamii, na kwenye maono ya pamoja kuhusu uwezeshaji kupitia mifumo ya kidijitali. Uzoefu wake unakamilisha uwezo wa Mkurugenzi katika masuala ya kifedha na mikakati, hivyo kutuwezesha kujenga timu ya uongozi iliyo imara, yenye uwiano na ufanisi katika kuendeleza SOHEECO PROJECTS. Uzoefu wake katika mahusiano unakamilisha Timu ya SOHEECO Projects na kuifanya itimize dhamira yake.
Ni mke wa mume mmoja (1) na mama wa mtoto mmoja (1).